Pages

Thursday, April 6, 2017

NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, AHMAD KASSIM HAJI AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI CHA KUANZISHWA MAFUNZO MAALUM YA KINGA YA MSINGI MASKULINI KUTOA ELIMU KWA WANAFUNZI KUJIKINGA DHIDI YA UHALIFU NA DAWA ZA KULEVYA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Nd. Ahmad Kassim  Haji (katikati aliyevaa Suti nyeusi) akikiongoza Kikao cha maandilizi ya kuanzishwa mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la  kutoa elimu itakayowasaidia wanafunzi kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya. (Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ) 
Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya     (UNODC) Bibi Sylvie Bertrandwa Pili kutoka kushoto akifafanua jambo juu ya mpango huo utakaosimamiwa na UNODC.

Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/4/2017.
UONGOZI wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya (UNODC), umeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika  kuanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la  kutoa elimu itakayowasaidia kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.

Uongozi huo umekutana na  Watendaji wa Tume ya Udhubiti wa Dawa za Kulevya pamoja na wale wanaosimamia udhibiti wa uhalifu Chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrand alisema mpango huo wa Mafunzo utashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Bibi Sylvie alisema katika kuupanguvu zaidi mpango huo ili ufanikiwe vyema Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto pia itakuwa mshirika katika mpango huo utaoratibiwa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar.


No comments:

Post a Comment