Pages

Sunday, March 19, 2017

Wenger kutangaza hatma yake hivi karibuni

Arsene WengerHaki miliki ya pichaPA
Image captionArsene Wenger
Hivi karibuni Meneja wa Arsenal Arsene Wenger atatangaza ikiwa atasalia Arsenal baada ya kufanya uamuzi wa hatma yake.
Wenger alikuwa akizungumza baada ya Arsenal kushindwa kwa mabao 3-1 na West Broms ambacho ni kipigo cha nnne kwa miaka mitano.
Kushindwa huku kulimuongezea shinikizo Wenger na kuiacha Arsenal katika hatari ya kushindwa kumaliza katika nafasi ya timu nne za kwanza kwa mara ya kwanaa kabisa tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 1996.
"Ninajua kile nitakifanya, hivi karibuni mtajua." alisema Wenger.
Mashabiki wamekuwa wakibeba mabango ya kumtaka Wenger kuondokaHaki miliki ya pichaPA
Image captionMashabiki wamekuwa wakibeba mabango ya kumtaka Wenger kuondoka
Mkataba wa Wenger unakamilika mwishoni mwa msimu lakini tayari ashaongezewa mkataba mpya wa miaka miwili.
Amekabiliwa na shinikizo siku za hivi karibuni huku mashabikia wakilalamikia kushindwa kwa Arsenal kwenye Premier League, na kushindwa na Bayern Munich kwa jumla ya mabao 10-2 katika Champions League na kumtaka aondoke.
"Nafikiri tuna kazi kubwa lakini tunahitaji kuungana na kuangazia mechi zinazokuja, kwa sababu tuna mechi kubwa," Wenger alikiambia kituo cha Sky Sports.
Arsenal walishindwa kwenye Premier League, na pia kushindwa na Bayern Munich kwa jumla ya mabao 10-2 katika Champions LeagueHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionArsenal walishindwa kwenye Premier League, na pia kushindwa na Bayern Munich kwa jumla ya mabao 10-2 katika Champions League

No comments:

Post a Comment