TANGAZO


Thursday, March 9, 2017

Wakili roboti awashauri wahamiaji kujaza maombi ya uhamiaji

Wakili robotiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAwali ''wakili roboti'' iliundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondoka kwenye maeneo ya kuegesha magari ama kupata tiketi za mwendo kasi.
Awali teknolojia ilitumiwa kukabiliana na faini za makosa ya bara barani sasa inawasaidia wakimbizi wenye madai ya kisheria.
Wakati Joshua Browder alipotengeneza DoNotPay aliita "Wakili roboti wa kwanza duniani".
Ni chatbot -programu ya kompyuta inayofanya mazungumzo kwa njia ya ujumbe na maagizo ya sauti - na inatumia ujumbe wa Facebook wa Messenger kukusanya taarifa juu ya jambo na kutoa ushauri pamoja na nyaraka za kisheria.
Joshua Browder aliyebuni programu ya DoNotPayHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAliyebuni programu ya DoNotPay - Joshua Browder anasema alivutiwa kubuni mfumo huo wa kisheria wa ushauri kwa wahamiaji kwasababu bibi yake alikuwa mkimbizi kutoka Austria wakati wa vita vya Holocaust
Awali iliundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondoka kwenye maeneo ya kuegesha magari ama kupata tiketi za mwendo kasi.
Lakini sasa Browder - Muingereza mwenye umri wa miaka 20-ambaye sasa anasoma katika chuo kikuu cha Stanford nchini Uingereza - ameweza kuwezesha roboti yake kuwasaidia wanaoomba uhamiaji.
Nchini Marekani na Canada, inawasaidia wakimbizi kukamilisha maombi yao ya uhamiaji, na nchini Uingereza, inaweza kuwasaidia wanaoomba uhamiaji katika kupata usaidizi wa kifedha kutoka kwa serikali.
Chatbot ya mawasiliano ya ''Wakili roboti''Haki miliki ya pichaJOSHUA BROWDER
Image caption''Wakili roboti'' inapofahamu kwamba mtumiaji anaweza kuomba uhamiaji, huchukua mamia ya maelezo na kujaza moja kwa moja maombi ya uhamiaji.
Programu ilitengeneza chatbot kwa kusaidiwa na mawakili kutoka kila moja ya nchi hizo.
"hufanya kazi kwa kuuliza msururu wa maswali kubaini kama mkimbizi anapaswa kulindwa na sheria za kimataifa ,"Aliimbia BBC , "kwa mfano: 'una hofu ya kuteswa katika nchi yako unakotoka ?'
"inapofahamu kwamba mtumiaji anaweza kuomba uhamiaji, huchukua mamia ya maelezo na kujaza moja kwa moja maombi ya uhamiaji.
Umuhimu wake ni kwamba maswali yote ambayo roboti hiyo huuliza ni ya kiingereza kinachoeleweka na akili yake bandia hutengeneza majibu ambayo huonekana wakati wa mazungumzo."
Roboti hupendekeza majibu ambayo mtumiaji anaweza kuyachagua ili kupunguza uwezekana wa maombi yake kukubaliwa, kwa mfano: " Jibu zuri kuhusu hali yako litajumuisha maelezo juu ya ni lini unyanyasaji ulianza katika nchi unakotoka."

No comments:

Post a Comment