Waajiri wana haki ya kuwapiga marufuku wafanyakazi, kuvaa vazi la hijab au vazi lolote linalovaliwa kwa misingi ya kidini au kisiasa, kutokana na uamuzia uliotolewa na mahakama ya juu barani Ulaya.
Lakini marufuku hiyo ni lazima itaambatana na sherehe ya kampuni husika ya kutaka waajiriwa wote kuvaa kwa njia ya kawaida, ilisema mahakama hiyo ya Ulaya ya ICJ.
Huu ndio uamuzi wa kwanza wa mahakama hiyo unaohusu suala la vazi la kiislamu la hijab.
Mahakama ya Ubelgiji ilipeleka kesi hiyo kwa mahakama ya juu barani Ulaya kwa uamuzi.
- Kenya: Mahakama yawaruhusu wasichana wavae hijab shule
- Msomali M'marekani awania taji la bi Minnesota
- Mfuasi wa Trump amshambulia Muislamu Marekani
Samira Achbita, alifutwa kazi baada ya kuanza kuvaa hijab kuenda kazini miaka mitatu baada ya kuajiriwa.
Alidai kuwa alikuwa akibaguliwa kwa misingi ya kidini.
Lakini kampuni aliyokuw akiifanyia kazi ilikuwa imefanyia sheria zake mabadiliko, na kuwazuia wafanyakazi kutokana na kuvaa vazi linaloonekana, linaloashiria dini yao au kwa misingi ya kisiasa.
Mahakama ya EU ilisema kuwa uamuzi huo haukuwa wenye ubaguzi wowote.
No comments:
Post a Comment