Taarifa ya Twitter iliyotumwa na mwandishi maarufu wa India kumuaibisha polisi mmoja wa nchi hiyo kwa kuwa mnene kupindukia imekuwa na matokeo ambayo hayakutarajiwa- Kupata huduma bure ya upasuaji wa kupunguza uzito mjini Mumbai.
Inspector Daulatram Jogawat left the hospital on Monday, and thanked Shobhaa De for making him famous.
Mwandishi alituma ujumbe wa Twitter wa picha ya Bwana Jogawat mwezi uliopita, akisema kuwa polisi huyo aliyeko Mumbai alikuwa na mpango wa "kuweka usalama mzito" kwa ajili ya uchaguzi wa mitaa. Ujumbe huo uliosambazwa sana uliifanya hospitali ya Saifee kujitolea kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wake.
Hospitali hiyo ilisema kuwa Inspekta Jogawat anaendelea vema baada ya upasuaji, na uzito wa mwili wake unaweza kupungua hadi karibu kilo 80 katika mwaka ujao. Alikuwa na uzito wa kilo 180 kabla ya upasuaji.
Upasuaji huo kwa lugha ya kitaalam -Bariatric surgery, hutumiwa kama tiba ya mwisho kwa mtu mwenye unene wa kupindukia unaoweza kumsababishia madhara ya kiafya.
Hospitali ya Saifee iligonga vichwa vya habari mwezi January ilipoanza shughuli zake kwa kumtibu mwanamke mmoja raia wa Misri, ambaye aliaminiwa kuwa mtu mwenye uzito mkubwa zaidi duniani akiwa na uzito wa mwili wa kilo 500.
Bwana Jogawat aliliambia gazeti la Hindustan Times kwamba alipata "fursa ya kwenda Mumbay kwa mara ya kwanza kwa ajili ya Matibabu" kwasababu ya ujumbe wa Tweeter.
Aliongeza kusema kuwa uzito wa mwili ulianza kuongezeka kutokana na matatizo ya kiafya, na si kwasababu anakula sana.
"kusema ukweli, uzito wangu haukuja kutokana na kazi yangu kwasababu nilikuwa mwenye nguvu na mkakamavu kimwili na nilikuwa na akili ya kutatua uhalifu. Nilikuwa nalipwa vema na kazi yangu," Alisema Bwana Jogawat.
Baadae mwandishi wa habari Shobhaa De baadae alitetea ujumbe wake wa Twitter, akisema kuwa azma yake haikuwa kumuudhi yeyote.
No comments:
Post a Comment