Baada ya kupata ushindi katika pambano lake dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu bondia David Haye, bondia Tony Bellew amesema yawezekana ikawa ndio muda wake wa kuamua kupumzika kuendelea na mchezo huo.
David Haye na bondia Tony Bellew walipigana katika pigano lililofanyika jumamosi kwenye ukumbi wa O2 Arena, Jijini London.
Katika mchezo huo Haye alionekana kushindwa kusimama vyema kutokana na kuumia vibaya mguu wake wa kulia, lakini alipambana hadi raundi ya 11 pale kambi yake ilipoamua kutupa taulo jeupe ili kuomba kumalizwa kwa pambano hilo.
Bondia David Haye amelazimika kufanyiwa upasuaji wa msuli nyuma ya mguu ni mara baada ya kuumia katika pambano lililomkutanisha dhidi ya bondia Tony Bellew huko London.
Katika pambano hilo David Haye aliumia misuli ya mguuni katika raundi ya sita na hivyo kujikuta akipigwa vikali na kushindwa kuendelea na pambano katika raundi ya 11.
Mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo muwakilishi wa David amewashukuru wale wote waliomtumia ujumbe wa pole na kumtia nguvu, pamoja na jopo la madaktari kutoka katika hospitali waliyomfanyia upasuaji.
Kwa upande wake Tony Bellew amesema alivunjika mkono katika pambano hilo japo alikuwa hasikii maumivu hata kidogo.
Amesema alivunjika mkono huo katika raundi ya pili au raundi ya tatu katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Uingereza BBC.
No comments:
Post a Comment