TANGAZO


Thursday, March 2, 2017

Timu ya soka ya Tibet yanyimwa visa ya Marekani

Timu ya soka ya wanawake ya Tibet

Haki miliki ya pichaTIBET WOMEN'S SOCCER
Image captionTimu ya soka ya wanawake ya Tibet

Timu ya soka ya wanawake ya Tibet inadai kunyimwa visa ya Marekani kushiriki michuano ya vijana inayoandaliwa kila mwaka mjini Texas.
Wanadai waliambiwa ''hawana sababu nzuri'' ya kuzuru Marekani.
Wachezaji wengi ni wahamiaji wa Tibet wanaoishi India na walikuwa wamewasilisha ombi la visa ya Marekani katika ubalozi wa Delhi.
Chini ya utawala wa Trump , Marekani kwa muda imepiga marufuku watu kuingia nchini humo kutoka nchi saba. Lakini raia wa Tibet na Wahindi si miongoni mwao.
Cassie Childers, mkurugenzi mtendaji wa timu hiyo ya soka ya wanawake ya Tibet na raia wa Marekani , ameiambia BBC kwamba alikuwa ameungana na kundi la wachezaji 16 kwa mahojiano katika ubalozi tarehe 24 mwezi Februari.
''Nimegadhabishwa kwani tulipanga safari hii kwa miezi kadhaa. Ilikuwa ni wakati muhimu kwa kila maisha ya mchezaji, walipojulishwa kuhusiana na safari hiyo.
Ilikuwa wakati wao wa kujidhihirisha ulimwenguni kwamba wanawake kutoka Tibet wanau wezo wa kufaulu kwa lolote,''amesema.
Bi Childers ameongezea 'ameaibika' baada ya nchi yake kuwakataza ruzuku za visa wachezaji wa timu hiyo ya wanawake

Timu ya Tibet inatarajia mualiko kutoka nchi yoyoteHaki miliki ya pichaTIBET WOMEN'S SOCCER
Image captionTimu ya Tibet inatarajia mualiko kutoka nchi yoyote

Timu ya Tibet inatarajia mualiko kutoka nchi yoyote
Hata hivyo, hadhani kwamba kunyimwa kwa visa hizo zinahusiani na chochote kuhusiana na utawala wa Trump.
''Nilikuwa naogopa matokea kama hayo, kwani raia wa Tibet hutaabika kupata visa za Marekani ,'' alisema Childers.
Amesema timu yake ilikuwa katika hali nzuri licha ya pigo hilo.
''Wachezaji hawajaathirika , nilikuwa nimekufa moyo, lakini wakanitia nguvu. Natumaini nchi nyengine zitatualika , zinazowakubali raia wa Tibet. Lakini tutakusanyika katika mji wa India na kufanya mazoezi.''
Wanawake katika timu hiyo, wanamiliki vitambulisho vya India, ambavyo ni stakabadhi zinazotolewa na serikali ya India kwa wakimbizi, na pia hufanya kazi kama cheti chao cha usafiri.
Wachezaji wawili katika timu hiyo walikuwa na pasipoti ya India.
Wengine wanne waliokuwa raia wa Nepal pia walikuwa wametuma maombi ya visa huko Kathmandu , lakini bado hawajapata jawabu kutoka kwa viongozi wa Marekani.
Kiongozi wa Marekani aliambia shirika la Habari la AP kwamba hawazungumzii kuhusu kesi binafsi, lakini bado uamuzi wa Marekani haujabadilika , kwamba Tibet bado inatambulika kuwa sehemu ya China.
Timu hiyo ilitarajia kushiriki michuano ya kombe la Dallas, ambayo huandaliwa kila mwaka kwa timu za vijana kutoka kutoke ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment