Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei, Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na waadishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu kutoka Ofisi hiyo Hashim Njewele.
Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na waadishi wa habari kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo kuhusu hali ya mfumuko wa bei kutoka kwa Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo
kuhusu hali ya mfumuko wa bei kutoka kwa Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za
Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja (hayupo pichani) wakati wa
mkutano wake na waandishi hao, leo Jijini Dar es Salaam.
Na Frank Shija – Maelezo.
KASI ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania umeongezeka kwa kiasi
kidogo ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS), Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari mwaka 2017.
Ruth
amesema kuwa mfumuko huo umeongeka kutoka asilimia 5.2 mwezi Januari hadi
kufikia 5.5 mwezi Februari, 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3
kiasi ambacho hakina athari katika uchumi wa nchi.
“Ongezeko
hilo la mfumuko wa bei umeendelea kukua kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi
zingine za ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Uganda na Kenya ambazo
tunashabihiana kwa kiasi kikubwa”. Alisema Ruth Minja.
Kwa
upande wa mfumuko wa bei kwa bidhaa za Vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi
cha mwaka, umeongezeka hadi asilimia 9.3 kutoka asilimia 8.2 mwezi Januari,
2017, wakati badiliko la fahirisi kwa bei zisizo za vyakula limebaki kuwa
asilimia 3.6 kama ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.
Ameongeza
kuwa farihisi za bei zimeongezeka hadi 106.97 mwezi Februari,2017 kutoka 101.44
mwezi Januari, 2017 wakati mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji
baridi kwa mwezi Februarii,2017 zimeongezeka hadi asilimia 8.7 kutoka asilimia 7.6
ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.
“Mwenendo
wa fahirisi za bei za Taifa na Mfumuko wa Bei kutoka mwezi Februari 2016 hadi
mwezi Februari, 2017 umeendelea kuimarika
ambapo katika kipindi hicho, mfumuko wa bei umekuwa na mwenendo imara
kutoka asilimia 5.6 mwezi Februari, 2016 hadi asilimia 5.5
februari,2017,”alisema Kaimu Meneja huyo.
No comments:
Post a Comment