TANGAZO


Thursday, March 9, 2017

Tanesco kuwakatia umeme walio na madeni Tanzania

Tanesco kuwakatia umeme walio na madeni Tanzania
Image captionTanesco kuwakatia umeme walio na madeni Tanzania
Kampuni ya umeme nchini Tanzania (Tanesco) imewapa muda wa siku 14 wale walio na madeni la sivyo wakatiwe umeme.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Tito Mwinuka, aliuambia mkutano wa waandisi wa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam kuwa, wizara na mashirika mengine ya serikali yanadaiwa deni la dola milioni 2.3 huku shirika la umeme la Zanzibar (Zeco) likidaiwa dola milioni 56.8.
Siku ya Jumapili rais wa Tanzania John Magufuli aliiamrisha Tanesco, kuwakatia umeme walio na madeni makubwa ikiwemo serikali ya Zanzibar.
Hivi majuzi Rais Magufuli aliamrisha walio na madeni kukatiwa umeme
Image captionHivi majuzi Rais Magufuli aliamrisha walio na madeni kukatiwa umeme
Leo hii bwana Mwinuka alikataa kuzungumzia hali kuhusu Zanzibar.
Hivi majuzi wizara ya kawi ilisema kuwa Tanesco inadai deni la dola milioni 363, na serikali ilikuwa imeingia kwenye mazungumzo na benki ya dunia kuomba mkopo ili kuboresha huduma za Tanesco.
Tanesco imekuwa ikitegemea mafuta ghali wakati wa kiangazi.

No comments:

Post a Comment