Meneja
wakala wa barabara Mkoani Tanga (Tanroad) Mhandisi Alfred Ndumbaro
akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la
Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu.
|
Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth
Gina akitolea ufafunzi baada ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa
kikao hicho.
|
Wajumbe wakifuatilia hoja
zilizoainishwa kwenye makabrasa kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi
(CCM) Omari Kigua na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda
Mtondoo.
Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) Jumaa Aweso akifuatilia jambo kwenye kabrasha lake
wakati kikao hicho kikiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias
Mwilapwa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga
Daudi Mayeji katika wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Lushoto, Kazimbaya Makwega akiperuzi kabrasa kwenye kikao
hicho.
Mbunge wa Jimbo la Tanga
(CUF) Musa Mbaruku na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema)
Yosepher Komba.
Mbunge wa Jimbo la
Mkinga (CCM) Dustan Kitandula kushoto akiwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Rashid Gembe.
Mkuu wa wilaya ya Handeni
Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini kikao hicho.
Kulia ni Mbunge wa Jimbo
la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akifuatilia kikao
hicho.
Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatilia kwa umakini kikao
hicho.
Mwandishi Mwandamizi wa
Shirika la Utangazaji la TBC Mkoani Tanga,Bertha Mwambela akiandaa
taarifa za kikao hicho.
WAKALA wa Ufundi na Umeme Mkoani
Tanga (Temesa) wameagizwa kuwasilisha orodha ya majina ya wadaiwa sugu
wa taasisi mbalimbali za serikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine
Shigella ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwemo
kuharakisha ulipwaji wake.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela wakati wa
kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani hapa ambapo alisema wao
kama serikali ya mkoa hawapo tayari kuona wakala huyo akishindwa
kutekeleza wajibu wake ipasavyo kutokana na juhudi zao kurudishwa nyuma
kimaendeleo.
Katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio makubwa yenye tija
alimtaka Meneja wa wakala wa Ufundi na Umeme (TEMEMSA) Mkoa Tanga,
Mhandisi Margareth Gina kumpelekea idadi ya wadaiwa sugu na taasisi hiyo
ili kuweza kuangalia namna ya kuweza kupata malipo yao.
Hatua hiyo inafuatia taarifa ya Meneja wa Temesa Mkoa kuonyesha zipo
taasisi nyingi za Serikali zinazodaiwa fedha nyingi bila kuwepo jitihada
zozote za ulipwaji wa madeni hayo huku tasisi hizo zikiendelea kupatiwa
huduma na taasisi hiyo ya Serikali.
Alisema ifike wakati kwa taasisi zote za umma zinazopata huduma kutoka
kwa wakala huo wa ufundi na umeme wahakikishe wanalipa madeni yao kwa
wakati kabla majina hayo ya wadaiwa hao sugu hayaja wekwa
hadharani.
Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa majina ya wadaiwa wote sugu yaorodhoshwe bila ya kuoneana aibu na taasisi za Serikali ambazo
inadaiwa kuwa ndio vinara wakubwa wa kudaiwa ili kuweza kuangalia namna
ya kupunguza madeni hayo ambayo ni hatari kwa ukuaji wa wakala
huyo.
Awali akizungumza katika kikao hicho,Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis
Margareth Gina alisema temesa imekuwa ikitoa huduma bora kwa taasisi za
Serikali kutokana na kuwepo na wataalamu wengi waliobobea katika fani
mbalimbali huku wakishindwa kufikia malengo kutokana na kutolipwa na wateja wao.
Mhandisi Gina alisema ipo orodha kubwa ya majina ya wadaiwa sugu ambapo
ipo haja ya kuyaweka hadharani kama Mkuu wa Mkoa alivyoagiza na kufanya
hivyo kunaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kuweza na kukusanya
madeni hayo.
“Zipo taasisi za serikali zanadaiwa hadi milioni 100 na orodha yote ya
wadaiwa sugu ninayo na naweza kuyataja ila naona itakuwa kufedheheshana
tu mbele ya kikao hiki.”Alisema.
Aidha alisema taasisi za Serikali kwa asilimia kubwa zimekuwa miongoni
mwa wateja wanaoikwamisha temesa kuendelea na ufanisi wa shughuli zake
jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzina wa haraka kukomesha tabia
hiyo iliyozoeleka.
Kwa upande wake, katibu Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Saidi alisema
hakuna sababu ya kuficha wanaodaiwa lazima waorodheshwe na walipe madeni
yao kwa wakati ili temesa iweze kuendelea na majukumu
yake.(Habari kwa hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha)
No comments:
Post a Comment