TANGAZO


Wednesday, March 15, 2017

Rais wa Korea Kusini awatelekeza mbwa wake ikulu

Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".
Makundi ya kutetea haki za wanyama yamemlaumu rais wa Korea Kusini aliyeondoka madarakani Park Geun-hye, kwa kuwatelekeza mbwa wake wakati aliondoka ikulu
Mzozo huo unaibuka wakati Bi Park anaitwa kuhojiwa kufuatia kutajwa kama mshukiwa kwenye sakata kubwa ya ufisadi ambayo ilichangia kuondolewa kwake madarakani.
Alitimuliwa wiki iliyopita wakati mahakama ya katiba ilidumisha uamuzi wa kuondolewa kwake madarakani.
Korea Kusini itafanya uchaguzi wake wa urais tarahe 9 mwezi Mei.
Bi Park ndiye rais wa kwanza aliyechagulia kidemokrasia kuondolewa madarakani.
Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina Haki miliki ya pichaCARE / FACEBOOK
Image captionBi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".
Mwishoni mwa wiki Bi Park aliondoka ikulu ya rais ambayo inafahamika kam Cheong Wa Dae na kuelekea nyumbani kwake kwenye mtaa wa kifahari mjini Seoul.
Mbwa wake tisa hawakuwa miongoni kwa vitu alivyoandamana navyo.
Kundi la kupinga unyanyasaji wa wanyama linasema kuwa alikiuka haki za wanyama kwa kuwaacha nyuma.
Msemaji wa ikulu alikana madai kuwa Bi Park aliwatelekeza mbwa wake na kuliambia shirika la Reuters kuwa mbwa hao waliachwa nyuma kwa sababu haingekuwa vyema wao kuondolewa kwenye makazi yao.
"Aliwaambia wafanyakazi wa ikulu kuwa wawatunze mbwa hao na wawatafutia makao ikiwa itawezekana," msemaji wake alisema,
Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".
Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".
Korea Kusini imekuwa ikiongozwa na waziri mkuu Hwang Kyo-ahn tangu bunge lipige kura ya kumuondoa madarakani mwezi Disemba.
Tarehe ya uchaguzi wa rais ilitangazwa wakati wa mkutano wa mawaziri siku ya Jumatano
Wakati wa mkutano huo bwana Hwang alisema kuwa hatawania urais, hatua ambayo ilikuwa pigo kwa chama cha Conservative.

No comments:

Post a Comment