TANGAZO


Monday, March 6, 2017

ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NCHINI

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo  mara baada ya kuzindua wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeathimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Muuandaaji ya wiki ya wanawake duniani kwa Mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima wa kwanza kulia  akishuhudua jinsi mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa anachukuliwa vipimo vya afya yake.




Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro akiwa anaingia uwanjani tayari kwa  uzinduzi  Rasmi zoezi la kupima Moyo, Cancer, Kisukari, Macho, Magonjwa Sugu ya mfumo wa hewa Bure yanayofanyika Arusha katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid  yaliyoandaliwa na Phide Entertainment kushirikiana na wafadhili mbalimbali ambapo kilele chake ni siku ya wanawake duniani tar 8/3/2017


Habari picha na Woinde Shizza, Arusha
TATIZO la baadhi ya watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari, kansa, na shinikizo la damu.

Hayo yalisemwa na mtaalamu wa magonjwa ya yasiyoambukizwa kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha, Mt meru, Dk Beatrice Ngogi wakati wa zoezi la upimaji wa afya bure lililofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.

Akihojiwa na waandishi wa habari mtaalamu huyo alisema asilimia kubwa ya kundi la watu walioathirika na magonjwa yasiyoambukizwa ni kati ya umri wa miaka 45-60 na kudai kuwa  mtindo wa maisha ya watu umechangia kwa kiasi kikubwa  ongezeko la magonjwa hayo.

“mtindo wa maisha umekuwa ni tatizo kubwa kwetu ndio maana tunawasihi watanzania tufanye mazoezi  na kuzingatia mlo wenye utaratibu”alisema mtaalamu huyo

Hatahivyo,mtaalamu wa magonjwa ya kisukari katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani kilimanajro,DK Valeria Matei alisema kwamba  katika siku za karibuni watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa kisukari mbali na wazee ambao ilikuwa imezoeleka.

Alisema kwamba elimu ya afya ni muhimu sana itolewe katika jamii ya watanzania kwa kuwa wengi wanakumbwa na ugonjwa huo bila kujijua na wakishajitambua ugonjwa huo unakuwa umeshawathiri kwa kiasi kikubwa.

Doroth Kuziwa, ambaye ni mwathirika wa ugonjwa wa kisukari alisema ya kwamba alikuwa kubaini kuathirika na ugonjwa huo kwa muda mrefu huku akisisitiza kwamba vyakula vya wagonjwa wengi wa kisukari vimekuwa ghali hali ambayo inawafanya washindwe kumudu gharama hizo.

Hatahivyo,Hiza Omary ambaye ni mgonjwa wa macho alisema kwamba aliacha kazi ya udereva kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya macho huku akisema kwamba vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuhabarisha umma kuhusu elimu ya afya katika jamii.

Mkurugenzi wa kampuni ya Phide Entertainment,Phidesia Mwakitalima alisema kwamba kampuni yake imeingia mkataba na hospitali za KCMC  na Mt Meru kwa lengo la kufadhili  zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa mkoa  wa Arusha  katika kuelekea siku ya wanawake duniani.

Alisema kwamba zoezi hilo litahitimishwa siku ya kilele cha siku ya mwanamke duniani  huku akisisitiza kundi la wanawake kuzingatia mfumo wa ulaji wa vyakula mbalimbali ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa.


Mmoja wa madaktari wanaotoa huduma akiwa anachukuwa damu salama kutoka kwa mwananchi ambaye amejitolea kuchangia damu.
Mmoja wa daktari akimpongeza mamaa mara baada ya kupimwa na kukutwa anaugongwa wa presha.
Dokta kutoka katika hospiotali ya kcmc akitoa elimu kwa wamama waliouthuria kupata huduma ya kupimwa bure.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro Akisaini Daftari la Wageni la Phide Entertainment baada ya Uzinduzi wa Zoezi la kupima buree wananchi Moyo, Cancer, Kisukari, Macho na Magonjwa sugu ya mfumo wa Hewa .. Pamoja na changizo la Damu kwa ajili ya Ward za Wazazi Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment