Catherine amesema kampuni ya MeTL imeamua kuweka utaratibu huo wa kuweka usawa kwa wafanyakazi kati ya wanaume na wanawake ili kuwapa nafasi wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo lakini pia kuepusha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kazini.
Mwakilishi wa MeTL Group, Catherine Decker akizungumza katika kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake.
“Kama kampuni tunatambua umuhimu wa usawa katika kuepusha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, sera hii inatusaidia katika kuwafatilia wafanyakazi wetu lakini pia inatutengenezea mazingira mazuri ya kupambana na matatizo kama ya utovu wa nidhamu na vitendo vya unyanyasaji ya kijinsia.”
Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano hilo.
“Itambulike kuwa MeTL sio tu mwajiri wa wafanyakazi hawa au kampuni bali ni familia moja ambayo inalenga kuboresha maisha ya watu kwa viwango mbalimbali na huwa tunaanda matukio ya michezo ambapo wanaume na wanawake hukutana na kushiriki vyema,” amesema Catherine.
Mbunge wa Urambo, Magreth Sitta kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake.
“Wanawake ni vyema mkashirikiana na wanaume, kama kuna jambo mnawambia ili kulifanya kwa pamoja, hata mimi siri ya kufika hapa nilipo ni sababu ya kuwashirikisha, mkifanya hivyo mtakuwa mmefanya jambo jema sana,” alisema Magreth.
No comments:
Post a Comment