Zaidi ya watu 30 wameuawa na maporomoko ya taka kwenye eneo moja kubwa la kumwaga taka nje ya mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.
Inaripotiwa kuwa watu kadha bado hawajulikani waliko tangu maporomoko hayo yatokee siku ya Jumamosi usiku.
Inaaminiwa kuwa watu takriban 150 walikuwa eneo hilo.
Mabanda kadha ya watu kwa sasa yamefukiwa chini ya tani kadha za taka.
Eneo hilo limekuwa likitumiwa kutupa taka kutoka kote mjini Addis Ababa kwa zaidi ya miongo mitano.
Watu wengi wamekuwa wakisaka eneo hilo kujitafutia riziki huku wengine wakiwa ni wenyeji.
Serikali nayo imekuwa ikijenga kiwanda cha kwanza kabisa barani Afrika, kwa lengo ya kuibadili taka hiyo kuwa nishati karibu na eneo hilo.
Wana mpango ya kuchoma taka kutoka mjni Addis Ababa na kuugeuza kuwa umeme
No comments:
Post a Comment