Raia wa Japan wa umri wa miaka 50 ameweka rekodi mpya ya kuwa mtu wa umri mkubwa zaidi kufunga bao katika mechi ya soka ya ushindani.
Kazuyoshi Miura aliweka rekodi hiyo kwa kufunga bao la pekee wakati wa ushindi wa 1-0 wa Yokohama FC dhidi ya Thespa Kusatsu katika ligi ya daraja la pili nchini Japan.
Rekodi ya awali iliwekwa mwaka 1965 na Mwingereza Stanley Matthews, aliyefunga bao lake la mwisho mechi ya ushindani akiwa na umri wa miaka 50 na siku tano.
Miura anamzidi umri kwa siku tisa.
Miura, ambaye aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Japan na kuwafungia mabao 55 katika mechi 89, kwa sasa anacheza soka msimu wake wa 32.
Alistaafu soka ya kimataifa miaka 17 iliyopita.
Miura wakati mmoja alicheza soka ya kulipwa Ulaya.
Alianza uchezaji wake akichezea Santos ya Brazil na akacheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa mwaka 1986.
Alichezea Genoa na Dinamo Zagreb miaka ya 1990.
No comments:
Post a Comment