TANGAZO


Friday, March 10, 2017

Je dunia itaifanya nini Korea Kaskazini?

Korean Kaskazini ilirusha makombora manne mapema mwezi huuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKorean Kaskazini ilirusha makombora manne mapema mwezi huu
"Taifa korofi ambalo ni hatari," Korea Kaskazini imetajwa kwa majina ya kila aina.
Serikali imelaumiwa kwa kuwandamiza vibaya raia huku ikiendelea na mipango ya kuunda silaha za nuklia.
Miezi ya hivi karibuni ilifanya jaribio la tano la kombora la nuklia, ikarusha makombora kadha huku wengi wakiamini kuwa ilimuua ndugu wa kambo wa kiongozi wa nchi hiyo kwa kutumia silaha ya kemikali.
Lakini mbona Korea Kaskazini ni tatizo, na ni kwa nini suluhu haliwezi kupatikana?
Historia
Korea Kaskazini ilibuniwa wakati rasi ya Korea ilitenganishwa mara mbili baada ya vita vya kati ya mwaka 1950 na 1953 vya Korea.
Kiongozi wake alikuwa ni Kim II-sung, mkoministi ambaye alitawala kwa kutumia chama kimoja ambaye ni babu yake kiongozi wa sasa Kim Jong-un.
Inasalia kuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani. Uchumi wake unadhibitiwa na serikali huku raia wake wakiwa hawana uwezo wa kufuatilia vyombo vya habari vya kigeni, na wakiwa pia hawana uhuru wa kutoka nje nchi hiyo isipokwa watu wachahe tu.
Cha kushangaza ni kuwa Korea Kaskazini imefanya majaribio matano ya nuklia na mengine kadha ya makombora, ishara ya kuendelea na lengo la kuunda bomu la nuklia.
Kim Jong-un (kati kati )Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKim Jong-un (kati kati )

Kuhusu mazungumzo

Kumekuwa na mazungumzo kadha huku ya hivi punde yakiwajumuisha China, Korea Kusini, Japan, Urusi na Marekani, ambayo yalionekana kuwa yenye matumaini.
Korea Kaskazini ilikubali kuachana na mipango yake ya nuklia ili iweze kupewa misaada. Makubaliano hayo yalichangia Korea Kaskazini kulipua kinu chake kilicho Yongbyong.
Lakini tena mambo yakaenda mrama. Marekani ilidai kuwa Korea Kaskazini imekataa kifichua kiwango cha mipango yake ya nuklia, Korea Kaskazini ikapinga hilo na tena ikafanya jaribio la nuklia.
Tangu mwaka 2009 hakujakuwa na mazungumzo yaliyo ya maana.

Shinikizo za kiuchumi

Umoja wa mataifa na nchi kadha bado zimeiwekea Korea Kaskazini vikwazo, zikilenga mipango yake ya silaha na uchumi. Vikwazo vya hivi punde ilivyowekewa ni vya kuagiza kutoka nje mkaa wa mawe.
Msaada ya chakula kuenda Korea Kaskazini ambayo inategemea misaada ili kuwalisha watu wake imepungua miaka ya hivi karibuni.
Korea Kaskazini imewekewa vikwazo vya kuagiza mkaa wa maweHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini imewekewa vikwazo vya kuagiza mkaa wa mawe
Kuna uwezekano wa kijeshi?
Inaaminika kuwa hatu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini zitasababisha maafa makubwa kwa wanajeshi na raia.
Kupata na kuharibu mirundiko ya silaha za nuklia nchini Korea Kaskazani itakuwa vigumu.
Wataalamu wanadai kuwa silaha zingine zimefichwa mbali chini ya ardhi. Kando na hilo Korea Kaskazini imejihami vikali hali inayoiweka hatarini Korea Kusini kutoka kwa silaha za kemikali na kibaolojia na takriban wanajeshi milioni moja.
Mauaji je?
Miezi ya hivi karibuni Korea Kusini imekuwa ikizungumzia kuhusu hatua ya kumuondoa madarakani Kim Jong-un.
Lakini lengo la Korea Kusini ni kuileta Korea Kaskazini kwenye meza ya mazungumzo kwa kuifanya kuhisi kuwa isiyo na usalama.
Lakini kuna maswali mengi kuhusu ni nani atajaza pengo ikiwa mauaji yatafanyika kwa kuwa hakuna upinzani nchini Korea Kaskazini.
Korea zote zina silaha na wanajeshi tayari kwa mzozo wowoteHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea zote zina silaha na wanajeshi tayari kwa mzozo wowote

Suluhu bora ni lipi?

Inahitajika kuwa na ushirikiano kati ya Marekani, China, Korea Kusini na Japan. Lakini kwa sasa kuna uongozi mpya nchini Marekani na malumbano ya kisiasa nchini Korea Kusini. Uhusiano kati ya Japan, Korea Kusini na China sio mzuri, kutokana na masuala ya kihistoria. China nayo inapinga vikali kujengwa mitambo ya Marekani ya makombora ya kujikinga nchini Korea Kusini.
Ndio maana Korea Kaskazini inahisi kuwa ina fursa ya kuendelea na mipango yako.

No comments:

Post a Comment