TANGAZO


Wednesday, March 8, 2017

China yaitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora

Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya makombora manneHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKorea Kaskazini ilifanya majaribio ya makombora manne
China imependekeza kwamba Korea Kaskazini ipige marufuku majaribio yake ya makombora pamoja na teknolojia yake ya nyuklia ili kuzima wasiwasi unaoendelea.
Waziri wa maswala ya kigeni Wang Yi alisema kuwa kwa makubaliano hayo Marekani na Korea Kusini zitasitisha mazoezi ya kijeshi ya pamoja ambayo yanakasirisha Korea Kaskazini.
Ombi hilo linajiri baada Korea Kaskazini kufanyia majaribio makombora yake manne siku ya Jumatatu na kukiuka vikwazo vya kimataifa.
Ili kujibu hatua hiyo, Marekani imeanza kuweka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Thaad.Haki miliki ya pichaFEDERATION OF AMERICN SCIENTISTS
Image captionMfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Thaad.
Akizungumza kando kando ya mkutano wa kila mwaka wa bunge, bwana Wang alisema kuwa mgogoro huo wa Korea ni kama treni mbili zinazokwenda katika barabara moja huku zote zikikataa kutoa nafasi kwa mwengine kupita.
"je pande hizi mbili ziko tayari kugongana?, aliuliza.
''Usitishaji wa operesheni za kijeshi baina ya mataifa haya utakuwa hatua ya kwanza katika kumaliza wasiwasi na kuanzisha majadiliano'',alisema.

No comments:

Post a Comment