Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewaambia mashabiki wa Chelsea kwamba yeye bado ni "Number One" (Nambari Moja) baada yake kuzomewa wakati wa mechi ambayo mabingwa hao watetezi wa Kombe la FA walilazwa 1-0 uwanjani wa Stamford Bridge Jumatatu.
Mourinho, ambaye alifutwa kazi mara mbili na Chelsea, aliitwa 'Yuda' na mashabiki wakati wa mechi hiyo.
Hata hivyo, aliwajibu kwa kuwaelekezea vidole vitatu, ishara ya mataji matatu ya ligi aliyoyashinda akiwa na klabu hiyo.
Alisema baadaye: "Hadi wampate meneja ambaye atawashindia mataji manne ya Ligi ya Premia, mimi bado ni nambari moja.
"Hadi wakati huo, Yuda ndiye nambari moja."
Bao la ushindi la Chelsea mechi hiyo ya Jumatatu lilifungwa na N'Golo Kante dakika ya 51.
Manchester walimaliza mechi wakiwa wachezaji 10 baada ya Ander Herrera kuonyeshwa kadi nyekundu dakikaya 35.
Mourinho, 54, ndiye meneja aliyefanikiwa zaidi Chelsea baada ya kushinda mataji matatu vipindi viwili alivyokuwa Stamford Bridge mwaka 2005, 2006 na 2015.
Alisema: "Wanaweza kuniita wanavyotaka. Mimi ni mtaalamu. Natetea klabu yangu.
"Najivunia sana wachezaji wangu. Najivunia sana mashabiki wa Manchester United.
Mourinho hata hivyo alikataa kuzungumzia kadi nyekundu aliyoonyeshwa Herrera na badala yake akasema Michael Oliver ni "mwamuzi mwenye matumaini makubwa (ya kufana)".
Mwenzake wa Chelsea Antonio Conte hata hivyo alidai wachezaji wa United walimwandama Hazard wakati wa mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment