Mwanzilishi wa Saccos ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE), Dkt. Anna Matindi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kutoka Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi, leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Chama cha Vijana Wajasiriamali – Taswe, Bi. Adelaida Ngowi. Mkutano huo, unatarijiwa kufanyika tarehe 24 Machi, 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa, Osterbey huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze katika Sekta Binafsi."
Mwanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TASWE), Bibi. Leah Paul Dennis akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kutoka Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi, leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa Chama cha Vijana Wajasiriamali – Taswe, Bi. Adelaida Ngowi, Mwanzilishi wa Chama hicho, Bibi.Anna Matinde na Bi. Grace Kimaro. Mkutano huo, unatarijiwa kufanyika tarehe 24 Machi, 2017 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa, Osterbey huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze katika Sekta Binafsi.”
Wakiwa katika picha ya pamoja.
VIJANA zaidiya 1000
kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi kukutanishwa jijini Dar es Salaam
katika Mkutano wa Kimataifa utakaofanyika tarehe 24 Machi 2017, katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa,
Osterbay Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Mwanzilishi wa Chama cha
Kuweka na Kukopa cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TASWE), Anna
Matinde wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo, leojijini Dar es
Salaam.
Bibi. Matinde amesema kuwa TASWE
kwa kushirikina na Kikundi cha Kwaya ya Remnant Generation
wameandaa Mkutano maalum kwa ajili ya vijana wa Vyuo Vikuu kwa leongo la
kuwajengea uywezo na kuwabadilisha fikra ili watambue fursa zilizopo katika Sekta binafsi.
“Tarehe 24 mwezi Machi kutakuwa na Mkutano mkubwa wa Kimataifa ambapo vijana kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali watashirikina kujengewa uwezo”.
AlisemaMatinde.
Kwa upande wake Katibu wa Vijana Wajasiriamali kutoka
TASWE amaesema kuwa lengo kubwa la
mkutano huo, ni kuwakutanisha vijana na kuwapa elimu itakayowabadilisha mitazamo yenye lengo
la
kuwafanya wafikirie kujikita katika Sekta binafsi badala ya kutegemea kuajiriwa pindi watakapomaliza masomo yao, ya elimu za juu.
Aliongeza sambamba na kubadilisha mitazamo yao mkutano huo, utasaidia kuwaondolea msongo wa mawazo utokanao na ukosefu wa ajira pamoja na ukweli kwamba wahitimu wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku huku ajira zikikua kwa kasi ndogo.
“Takribani Vijana 1200
kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi wanatarajia kukutana ikiwa lengo kubwa ni kuwasaidia vijana hao na kutambua kuwa ujasiriamali ni sehemu ya ajira”,
alisisitiza Bi. Adelaida.
Mkutano huo, wa Kimataifa wa Vijana unaandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chama
cha Kuweka na Kukopa cha Wajasiriamali Wanawake Tanzania (TASWE) na Kikundi cha
Wanakwaya cha Remnant Generation kinachojali wahitaji kwa kusaidia mahitajiya.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Badilisha Mtazamo wa Vijana wajielekeze katika Sekta Binafsi”.





No comments:
Post a Comment