TANGAZO


Saturday, February 25, 2017

Tume yasema makaburi ya jumla yametapakaa Burundi

Makaburi ya jumla nchini Iraq
Image captionMakaburi ya jumla nchini Iraq
Tume ya ukweli na maridhiano nchini Burundi imesema inaamini kuna makaburi ya jumla ya watu zaidi ya elfu mbili mia tano yaliyotapakaa katika maeneo mengi ya nchi hiyo miongoni mwao yale ya kale mno.
Tume hiyo CVR, inayoungwa mkono na serikali ya Burundi , imesema makaburi hayo ni ya watu waliouawa kiholela tangu nchi hiyo ijinyakuliwe uhuru wake 1962, na wenyeji wa maeneo husika ndio waliowapa habari hizo.
Takriban watu elfu 2 wanasadikiwa kufariki katika mauaji ya 1972, na wengine laki tatu kuuawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 90s.
Wengine walifariki katika machafuko ya kisiasa ya hivi majuzi kutokana na uchaguzi wa utata wa Pierre Nkurunziza kwa muhula wa tatu.
Sasa tume hiyo inasema inakabiliwa na kibarua kigumu cha kupata fedha za kufanyia shughuli za ufukuaji wa makaburi hayo katika jitihada za kutambua wahanga na kubaini ukweli kuhusu vifo vyao.

No comments:

Post a Comment