TANGAZO


Sunday, February 12, 2017

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA KITAIFA KUFANYA MAZOEZI NA KUPIMA AFYA BILA MALIPO ILIYOANDALIWA NA WIZARA YA AFYA MJINI DODOMA

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima mapigo ya moyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo. JKCI inashiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya  bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma. 
Baadhi ya wanakamati wa  kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma wakitayarisha fomu za kujaza wananchi watakaofika katika uwanja huo kwa ajili ya  kupima afya zao bila malipo. 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Pedro Pallangyo akimpima ugonjwa wa kisukari Agnes Luberi aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo bila malipo huku wanafunzi wanaosomea kozi ya udaktari katika Chuo kikuu cha Dodoma wakiangalia. Zaidi ya wananchi 170 walifika katika banda hilo kwa siku ya kwanza ya upimaji kwa ajili ya kupima afya zao ili kujuwa kama wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo au la. 
Waandishi wa Habari wakichukua matukio mbalimbali katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo  kwa siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma  wakiwa katika mstari wa kusubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya  bila malipo kwa siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto na kufanyika  katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.  
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma  wakiwa katika mstari wa kusubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya  bila malipo kwa siku mbili iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto na kufanyika  katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.  
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Pedro Pallangyo akimweleze madhara ya magonjwa ya moyo mwananchi aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo bila malipo ili aweze  kujuwa kama anasumbuliwa na magonjwa ya moyo au la. (Picha zote na Anna Nkinda – JKCI)

No comments:

Post a Comment