Fundi wa kuchoma vyuma kwa kutumia teknolojia ya gesi
akiendelea na zoezi la kuchoma kufuli ya lango la ghala lililofichwa kwenye
hoteli ya Butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Ghala hilo
limekutwa na shehena kubwa ya kazi haramu za muziki na filamu.
Mmiliki wa ghala lilolokutwa chini ya hoteli ya
Butterfly, Phili Ulaya akijaribu kujitetea mbele za Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye mara baada ya zoezi la kuvunja kufuli ya lango la ghala
hilo kukamilika. Waziri Nape kwa kushirikiana na viongozi wa taasisi
zinazosimamia maslahi ya kazi za ubunifu wamefanya operesheni iliyofanikisha
kukamtwa kwa shehema kubwa ya kazi
haramu za filamu na muziki kwenye ghala la bwana Ulaya liliofichwa chini ya
hoteli ya Butterfly.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye akimfafanulia sheria mbalimbali ambazo mfanyabishara wa kazi za filamu
na muziki anastahiki kuzifuata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo.
Anaemsikiliaza Mheshimiwa Nape ni mmiliki wa ghala ambalo shehena kubwa ya kazi
haramu za filamu na muziki zimekamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika leo
eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Nnauye akikagua rundo la filamu zilizokamatwa kwenye opersheni ya kutokomeza
kazi haramu za filamu na muziki nchini. Kwenye operesheni hiyo shehena kubwa ya
kazi za filamu na muziki imekamatwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli
ya Butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo jijini Dar-es-Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Filamu wa
Bodi ya Filamu Tanzania Wilhad Tairo wakati wa operesheni ya kutokomeza kazi
haramu za filamu na muziki nchini. Operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa kwa
shehena kubwa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli
ya butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo.

No comments:
Post a Comment