TANGAZO


Saturday, February 25, 2017

Serikali: Ali Hassan Mwinyi ni mzima kama kigongo

Aliyekuwa rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na rais mpya wa taifa hilo Magufuli
Image captionAliyekuwa rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na rais mpya wa taifa hilo Magufuli
Serikali ya Tanzania imepinga uvumi uliokuwa ukienea kuhusu kifo cha aliyekuwa rais wa zamani wa taifa hilo Ali Hassan Mwinyi.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo, Mkurugenzi wa huduma za mawasiliano nchini humo Hassan Abbas alisema katika taarifa kwamba uvumi huo hauna msingi na kwamba raia wanafaa kuupuzilia mbali.
Gazeti hilo limemnukuu bwana Abbas akisema:''Mzee Mwinyi ni mzima kama kigongo na anaendelea na shughuli zake bila tatizo lolote.
''Siku ya Alhamisi alihudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa na ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania kuadhimisha siku kuu ya kitaifa ya Kuwait na leo{ Ijumaa} amemtembelea aliyekuwa waziri mkuu Cleopa David'',ilisema taarifa.
Aidha kulingana na The Citizen nchini Tanzania, Abbas aliwashauri watumiaji mitandao kuchukua tahadhari na habari wanazokutana nazo.
''Tusitumie vibaya mitandao ya kijamii'',alisema.
Pia aliongezea kuwa ni kinyume na sheria chini ya sheria ya uhalifu 2015 kwa mtu yeyote kuchapisha, kutangaza ama kutoa habari zozote zisizo na ukweli katika mitandao ya kijamii.
Kwa niaba ya serikali ,Abbas aliomba msamaha kwa bwana Mwinyi na familia yake pamoja na watu wengine ambao kwa njia moja ama nyengine waliathiriwa na uvumi huo.

No comments:

Post a Comment