TANGAZO


Monday, February 20, 2017

Mzozo waibuka kati ya Korea Kaskazini na Malaysia kufuatia kuuawa kwa Kim Jong-nam

Kuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKuuawa kwa Kim Jong nam kumezua mzozo wa kidiplomasia
Malaysia imechukua hatua za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskania kuafuatia kuuwa kwa Kim Jon-nam ndugu wa kambo wa kiongzia wa Korea Kaskazini Kim Jon-un.
Kim alifariki kwa njia ya kutatanisha wiki iliyopita kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.
Polisi wanaamini kuwa alipewa sumu.
Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia Kang Chol, anasema kuwa haamini uchunguzi wa Malaysia.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBalozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia Kang Chol, anasema kuwa haamini uchunguzi wa Malaysia.
Malaysia imemuita balozi wake kutoka mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang, na kumuita balozi wa Korea Kaskazini wakitaka maelezo.
Polisi nchini malaysia kwa sasa wanasema kuwa wanawatafuta watu wanne raia wa Korea Kaskazini.
Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia Kang Chol, anasema kuwa haamini uchunguzi wa Malaysia.
Mwanamume mmoja raia wa Korea Kaskazini tayari amekamatwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwanamume mmoja raia wa Korea Kaskazini tayari amekamatwa
Waziri mkuu nchi Malaysia ametetea polisi wa nchi hiyo na kusema kuwa anataka Korea Kaskazini kuelewa kuwa sheria inatumika nchini Malaysia.
Kanda moja ya video ambayo inaonyesha picha za CCTV za shambulizi dhidi ya Kim Jong-nam, imetokea na kupeperushwa na televisheni moja ya Japan.
Hong Song Hac, 34, na Ri Ji Hyon, 33, wanatafutwa na polisi wa MalaysiaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHong Song Hac, 34, na Ri Ji Hyon, 33, wanatafutwa na polisi wa Malaysia

No comments:

Post a Comment