Meli
ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), inayofanyiwa
ukarabati katika bandari ya Mwanza ambao ukarabati wake utakamilika mwanzoni
mwa wiki ijayo na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi huu.(Picha zote na Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U))
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Eric Hamisi (mwenye shati jeupe), wakati alipokagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias.
Fundi wa Kampuni ya
Huduma za Meli (MSCL), akiendelea na ukarabati wa meli ya MV Clarias ambayo
ukarabati wake utakamilika mwishoni mwa wiki na kuanza kazi ya kutoa huduma
katika Ziwa Victoria.
Nahodha wa Meli ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Swedi Ruganza akitoa maelezo ya namna nahodha anavyoendesha meli kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho (katikati), alipofanya ukaguzi wa ukarabati wa meli hiyo jijini Mwanza.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt.
Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli
(MSCL), Bw. Eric Hamisi
(wa pili kutoka kushoto), mara baada ya kuangalia kina cha maji katika bandari
ya Mwanza.
Na Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)
KATIBU Mkuu
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard
Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa kukarabati
meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha utendaji kazi wa kampuni
hiyo.
Akizungumza
jijini Mwanza mara baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo Eng.
Dkt. Chamuriho amesema Serikali itawekeza kikamilifu kwenye kampuni hiyo baada
ya kuridhika na utendaji uliopo sasa.
“Fanyeni kazi
kwa bidii na fikra mpya Serikali inashughulikia kwa karibu suala la mishahara
yenu na stahili nyingine” amesema Eng. Dkt. Chamuriho.
Hivi karibuni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alimteua Kaimu
Meneja Mkuu mpya wa kampuni hiyo Bw. Eric Hamisi ambaye kwa kushirikiana
vema na menejimenti na wafanyakazi wamewezesha kuongeza mapato kwa kwa asilimia
100.
Kampuni ya huduma za Meli MSCL ni moja
ya kampuni ya Meli yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na kusimamiwa
na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi na inatoa huduma za usafirishaji wa abiria na
mizigo katika maziwa makuu yaliyopo
nchini Victoria,Nyasa na Tanganyika

No comments:
Post a Comment