TANGAZO


Sunday, February 26, 2017

Malaysia yatangaza uwanja wa ndege kuwa salama baada ya kuuwa Kim Jong-nam

Wataalamu wakifanya uchunguzi uwanja wa Kuala LumpurHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWataalamu wakifanya uchunguzi uwanja wa Kuala Lumpur
Maafisa wa usalama wa Malaysia wametangaza kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur ni salama baada ya kuuawa kwa Kim Jong-nam.
Kim Jong-nam, kaka wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aliuawa katika uwanja huo siku 12 zilizopita.
Awali, polisi walipekua jengo husika wakichunguza iwapo kulikuwa na sumu kali iliyotumiwa katika mauaji hayo aina ya VX, au sumu nyingine yo yote.
Maelfu ya abiria wamepitia uwanja huo tangu kisa hicho kitokeeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaelfu ya abiria wamepitia uwanja huo tangu kisa hicho kitokee
Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.
Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliyofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.
Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa. Hadi sasa watu watatu wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo.
Kim Jong-namHaki miliki ya pichaAP
Image captionNorth Korea has not identified the man who died as Kim Jong-nam, only as a North Korean citizen
Siti Aisyah anasema alilipwa dola 90Haki miliki ya pichaEPA
Image captionSiti Aisyah anasema alilipwa dola 90

No comments:

Post a Comment