TANGAZO


Monday, February 27, 2017

Maduka ya wageni yaporwa Afrika Kusini


Maduka eneo la Jeppeston yanayomilikiwa na wageni yalivamiwa.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMaduka eneo la Jeppeston yanayomilikiwa na wageni yalivamiwa.

Polisi kwenye mji mkubwa zaidi nchini Afrika Kusini wa Johannesburg, wanasema kuwa karibu watu 100 walishiriki katika uporaji usiku kucha.
Maduka eneo la Jeppeston yanayomilikiwa na wageni yalivamiwa.
Milango na madirisha vilivunjwa ambapo chakula na bidhaa zingine kwenye maduka yanayomilikiwa na wageni vikimwagwa sakafuni.
Abdul Ebrahim, mmiliki wa duka ambaye ni raia wa Somalia, ambaye alikuwa amejificha ndani ya duka lake, anasema kuwa hafahamu ni kwa nini watu walimvamia.
Afrika Kusini imekuwa ikikumbwa na ghasia mpya na maandamano dhidi ya raia wa kigeni huku kundi linalipinga wageni likifanya maandamano wiki iliyopita mjini Pretoria.
Mashambulizi hayo yamekosolewa pakubwa barani Afrika, huku Nigeria ikitoa wito kwa Muungano wa Afrika ikiutaka uingilia kati.

No comments:

Post a Comment