Karibu polisi 2500 wanatumwa eneo la Kerio Valley magharibi mwa Kenya, kuwasaka wale wanaoshukiwa kuhusika kwenye mauaji ya watu 10 wakiwemo wanasiasa wawili pamoja na wizi wa mifugo.
Takriban watu wengine 4000, pia wamekimbia makwao sehemu hiyo.
Eneo hilo kawaida limekumbwa na ghasia kati ya makabila ya Pokot na Tugen waking'ang'ania malisho ya mifugo wao.
Wadadisi wanasema kuwa uchaguzi ambao utafanyika mwezi Agosti nao imechangia hali hiyo.
Naibu Rais William Ruto, ambaye alizuru eneo la Kerio Valley siku ya Jumatatu alesema kuwa dola 970,000 zitatumiwa kuwafidia wale waliopoteza mifugo wao kutokana na visa vya wizi wa mifugo hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment