Waziri mkuu wa Ivory Coast Daniel Kablan Duncan amejiuzulu na kuvunja serikali yake katika hatua ambayo ilitarajiwa kufuatia kuidhinishwa kwa katiba mpya na uchaguzi wa ubunge wa mwezi uliopita.
"Nimejiuzulu pamoja na serikali," alisema akiwa kwenye ikulu ya rais baada ya mkutano na rais Alassane Ouattara.
Upinzani ulisusia Uchaguzi wa ubunge miaka 5 iliyopita, kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyodumu miezi kadhaa, na kupelekea vifo vya watu 3000.
- Uchaguzi: Usalama waimarishwa Ivory Coast
- Ivory Coast ina katiba mpya
- 'Upendeleo' katika kesi ya Simone Gbagbo
Asilimia 42 ya wapiga kura walijitokeza kwenye zoezi la kuidhinisha katiba. Moja wapo ya kipengee kilichobadilishwa ni ulazima wa wagombea wa Urais kuwa na wazazi asilia wa nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment