Pages

Monday, January 9, 2017

Wanaoshukiwa kumpora Kim Kardashian wakamatwa

Kim Kardashian West anasema alihofu kuwa angeuawa wakati wa wizi wa mjini Paris

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKim Kardashian West anasema alihofu kuwa angeuawa wakati wa wizi wa mjini Paris

Watu 16 wamekamatwa kwa kuhusishwa na wizi wa kutumia nguvu uliomkumba msanii Kim Kardashian West mjini Paris mwezi Oktoba.
Utawala unasema kuwa msanii huyo raia wa Marekani aliporwa kwa nguvu na takriban watu wawili waliokuwa wamevaa sare za polisi.
Wanaume hao waliingia chumba cha kifahari alichokuwa Kim Kardashiana kabla ya kumfunga na kumfungia kweye bafu.
Kisha wanaume hao walitoroka na vito vya thamani ya dola milioni 10.5.
Polisi wa Ufaransa wanasema kuwa uchunguzi wa DNA ndio ulichangia kukamatwa kwa watu hao.
Wanaume hao waliakamatwa wakati wa uvamizi ulioendeshwa maeneo ya Paris, Normandy na la Frech Riviera kufutia uchunguzi wa miezi kadha.
Moja ya uchunguzi wa DNA ulikuwa sawa na ule wa mtu anayejulikana kwa polisi kuwa mhalifu.
Kardashian ambaye ni mke wa mwanamuziki Kanye West alisema alikuwa na hofu kuwa angeuawa wakati huo.
Kardashian mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 36 alikuwa mjini Paris kwa maonyesho ya mitindo.


Kanye West alisitsisha tamasha alipojulishwa kuwa mkewe ameibiwa

No comments:

Post a Comment