Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye
amekutana na wadau wa sekta filamu nchini na kuoneshwa kusikitishwa juu ya
shutuma dhidi yake na serikali kuwa wamekamata bidhaa haramu za wasanii na
kuzirudisha kwa wamiliki kupitia mlango wa nyuma.
Akiongea wakati alipotembelea moja ya ghala la Kampuni ya
Udalali ya YONO Waziri Nape amewatoa hofu wasanii na kuwaeleza kuwa bidhaa hizo
za muziki na video ziko mahali salama na zitateketezwa bila kificho muda si
mrefu
Akiongelea kuhusu sakata hilo Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba amewaasa wasanii kuacha tabia ya kushutumu
viongozi bila kuwa na ushahidi wa kutosha
Katika Ziara hiyo Waziri Nape aliongozana na Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo na Wawakilishi kutoka Mamlaka ya
Mpato Tanzania (TRA),COSOTA,Tume ya Ushindani wa Kibiashara(FCC) na Baraza la
Sanaa Tanzania (BASATA)
No comments:
Post a Comment