TANGAZO


Wednesday, January 25, 2017

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE, YASEMA GRIDI YA TAIFA IKO SALAMA


Kaimu Meneja Mwandamizi, Udhibiti Mifumo ya Umeme TANESCO, Makao Makuu, Mhandisi Abubakar Issa (katikati), akionyesha kifaa kilicholipuka (female connector), cha umeme wa 132kv kutoka Ubungo kwenda Chalinze. Kulia ni Kaimu Meneja Uhusiano, Bi. Leila Muhaji na kushoto ni Mwangalizi Mkuu wa Kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, Bw. Deodatus Ngwanda.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeeleza chanzo cha kukatika umeme leo Januari 25, 2017), ni kulipuka kwa kikata umeme (Circuit breaker), baada ya kifaa kijulikanacho kama 'female connector' ya umeme wa 132kv kutoka kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwenda Chalinze mkoani Pwani kupata hitilafu.


Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mwandamizi Udhibiti Mifumo ya Umeme TANESCO, Makao Makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(pichani juu), alisema hitilafu hiyo iliyotokea majira ya saa 12;32 asubuhi, leo Januari 25, 2017  ilileta athari kwenye mfumo mzima wa gridi ya taifa na kufanya wateja wa TANESCO walio kwenye mikoa inayotumia gridi ya taifa kukosa umeme kwa takriban masaa mawili.

"Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa gridi ya taifa iko salama, hakuna tatizo lolote isipokuwa ilizima baada ya kikata umeme hicho kulipuka, lakini sasa mambo yamewekwa sawa na umeme unazidi kurejea katika hali yake ya kawaida kote nchini" alisema Mhandisi Issa, wakati waandishi wa habari walipopelekwa kujionea wenyewe hitilafu hiyo majira ya mchana leo. 



Hata hivyo alisema kifaa kilichoharibika kinasafirishwa kutoka mkoani Tanga, na mara kitakapowasili kitafungwa mahala kilipoharibika kile cha awali.
Hii ndiyo kikata umeme (Circuit breaker), iliyolipuka.
'Female Connector' inayotoa umeme hapo ubunge kupeleka Chalinze, mkoani Pwani ambayo ililipuka.
'Female connector' (juu katikati) iliyolipuka.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Makao Makuu, Bi. Leila Muhaji, akiwa na baadhi ya waandshi wa habari waliotembelea eneo hilo leo mchana Januari 25, 2017.
Kaimu Meneja Mwandamizi, Udhibiti Mifumo ya Umeme TANESCO, Makao Makuu, Mhandisi Abubakar Issa (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kifaa kilicholipuka (female connector), cha umeme wa 132kv kutoka Ubungo kwenda Chalinze.

No comments:

Post a Comment