Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) Bw. Salim Msangi
akisoma taarifa ya utekelezaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) kuhusu Ujenzi wa jengo jipya la abiria
(Tb III), lililopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere JNIA. Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)
SERIKALI imesema
itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Abiria la Tatu la abiria (Terminal
III) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam ili kuboresha huduma za usafiri
wa anga nchini.
Akizungumza mara baada
ya kukagua mradi huo Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi huo
sehemu ya kwanza ilifadhiliwa na Benki ya HSBC ya Uingereza hivyo sehemu ya
pili Serikali itatoa fedha ili
kukamilisha mradi huo.
”Awamu ya kwanza ya
ujenzi huu tulipata mkopo lakini awamu ya pili ya mradi Serikali tumesema
hatutachukua mkopo, tutajenga kwa fedha zetu za ndani sababu tuna uzoefu mkubwa
wa utekezaji wa miradi kwa kutumia fedha za zetu za ndani'' amesema Prof.
Mbarawa.
Aidha, Prof. Mbarawa
ameongeza kuwa imarishaji wa viwanja vya ndege nchini unakwenda sabamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) ambao mpaka sasa tayari lina ndege mbili aina ya Bombadier
Q400.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi , amesema
mpaka mwishoni mwa mwanzoni wa Mwaka huu mradi huo umekamilika kwa asilimia 66
na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kuezeka na kumalizia kazi za ndani ya jengo
ikiwemo usimikaji wa mitambo ya umeme, viyoyozi na utandikaji wa nyaya na
mbomba kwa ajili ya miundombinu ya ndani.
Ameongeza kuwa kazi za
nje ya jengo zinazohusisha maegesho ya
ndege yamekamilika kwa asilimia 53, maegesho ya magari asilimia 36 na eneo
la mitambo na umeme asilimia 46.
Bw. Msangi amesema
kuwa mpaka kufikia mwaka 2020 idadi ya abiria wanaotumia kiwanja cha JNIA
watafikia milioni 5 kwa mwaka na makadirio ifikapo mwaka 2025 idadi itaongezeka
watafiia milioni 5 kwa mwakaa.
Mradi huu wa jengo la
mita za mradi za mraba sitini elfu unatarajiwa kukamilikak mwezi Desemba Mwaka
huu na utahudumia abiria zaidi ya milioni 6 kwa mwaka na litaweza kuhuduumia
abiria 2,700 kwa saa na litakuwa na uwezo wakuhudumia ndege kubwa aina ya
Airbus A380.
No comments:
Post a Comment