TANGAZO


Wednesday, January 25, 2017

Philippe Countinho asaini mkataba mpya Liverpool

Philippe Coutinho (katikati)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.
Countinho atapokea kitita cha pauni 150,00 kwa wiki, na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa kiwango cha juu zaidi katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil mwenye miaka 24, alijiunga na majogoo hao wa Anfield kutoka Inter Milan kwa pauni milioni 8.5 mwezi Januari mwaka 2013.
Mkataba huu mpya utamfanya mshambuliaji huyo kusalia na klabu hiyo hadi mwaka wa 2022.
Coutinho amefunga mabao 34 katika mechi 163 alizoshiriki na Liverpool.
''Ni klabu ambayo naishukuru sana, ndiyo inayodhihirisha furaha yangu hapa,'' aliiambia mtandao wa klabu hiyo.
Hakuna kifungu chochote kuhusu kuondoka kwake kwenye mkataba wa Countinho, ambao utaanza kutekelezwa rasmi mwezi Julai.
Mshambuliaji wa Liverpool Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Countinho alisemekana alikuwa na matamanio ya kuihamia klabu ya Uhispania ya Barcelona.
''Nimesaini mkataba huu mpya kusalia na klabu hii kwa miaka mingine kadhaa, kwa sababu ni heshima kubwa kwangu.
''Nafasi hii imenipatia furaha, kwa sababu nilikaribishwa kwa mikono miwili na kila mmoja katika klabu hii na pia mashabiki tangu siku yangu ya kwanza.''
Coutinho alinunuliwa na meneja wa zamani Brendan Rodgers, wakati Southampton pia walipotaka kumsajili wakati huo.
Mshambuliaji huyo alijiwasilisha kama kiungo muhimu wa Reds kwa miaka minne huko Anfied.
Coutinho amerudi uwanjani baada ya kuugua jeraha la kifundo cha mguu, ambapo hapo awali alikuwa amefunga magoli sita katika mechi 14 alizoshiriki msimu huu.

No comments:

Post a Comment