TANGAZO


Monday, January 23, 2017

Note 7: Samsung yasema betri zilikuwa na kasoro


Galaxy Note 7Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu takriban 2.5 milioni walikuwa wamenunua simu za Galaxy Note 7

Uchunguzi uliofanywa na Samsung kuhusu visa vya simu aina ya Galaxy Note 7 kushika moto, umebaini kwamba visa hivyo vilitokana na kasoro kwenye betri.
Kampuni hiyo iliacha kutengeneza na kuuza simu hizo Oktoba mwaka jana baada ya visa hivyo kuripotiwa kwa wingi.
Simu ambazo zilitolewa upya pia zilikuwa zinashika moto.
Lakini Jumatatu, Samsung imesema tatizo halikutokana na programu za simu hiyo iliyotarajiwa kutoa ushindani kwa simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple.
Aidha, Samsung wamesema kasoro haikuwa kwenye sehemu nyingine za simu hiyo ila kwenye betri pekee.
Hatua ya kuzichukua tena simu zote zilizokuwa zimeuzwa inakadiriwa kuigharimu kampuni hiyo ya Korea Kusini jumla ya $5.3bn (£4.3bn) na kuathiri pakubwa sifa za kampuni hiyo.
Uchunguzi wa ndani na uchunguzi huru "umebaini kwamba betri ndizo zilizokuwa chanzo cha moto katika Note 7," Samsung imesema kwenye taarifa.
Kampuni hiyo imesema kasoro kwenye uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa betri hizo, zilisababisha betri hizo ambazo ziliundwa na kampuni mbili kuwa na kasoro.

Samsung Note 7 adHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya wachanganuzi walikuwa wamesema Note 7 ilikuwa simu bora zaidi ya Android kuwahi kuundwa

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi, matatizo yanatokana na betri hizo kuwa kubwa na hivyo kutotoshea vyema kwenye sehemu yake ndani ya simu.
Aidha, hakukuwa na nyenzo za kutosha za kukinga betri hizo dhidi ya joto.
Samsung imesema inawajibika kutokana na "kukosa kwetu kutambua na kuthibitisha matatizo yaliyotokana na muundo wa betri na kasoro kwenye uundaji wa betri."

No comments:

Post a Comment