Neymar ndio mchezaji mwenye thamani ya juu barani Ulaya akiwa na pauni milioni 216 kulingana na utafiti mpya ambao pia unatoa thamani ya wachezaji kumi walio na thamani ya Yuro milioni 100.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona amempiku mchazaji mwenza katika klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye ana thamani ya pauni milioni 149.
Mchezaji wa pekee kutoka Uingereza aliyeorodheshwa miongoni mwa wachezaji 10 walio na thamani ya juu duniani ni mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane mwenye thamani ya pauni 122 na Dele Alli mwenye thamani ya pauni milioni 96.
Paul Pogba ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United kwa rekodi ya kitita cha pauni milioni 89 ana thamani ya pauni milioni 136.4.
Utafiti huo umefanywa na kundi moja la wasomi kutoka CIES.
Walitafuta thamani hiyo kupitia viwango vya uchezaji wa wachezaji hao, kama vile umri na urefu wa kandarasi.
Cristiano Ronaldo, mshindi wa taji la mchezaji bora duniani yuko katika nafasi ya saba akiwa na thamani ya pauni milioni 111, huku kiungo wa kati wa Real Madrid Gareth Bale akiwa katika nafasi ya 14 na thamani ya pauni milioni 73.8.
Pogba ni mchezaji wa pekee aliyeko miongoni mwa 5 bora ambaye hachezei klabu ya Uhispania huku Antoine Griezman akiwa katika nafasi ya tatu na thamani ya pauni milioni 132 naye mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez akiwa wa tano na thamani ya pauni milioni 127.
Kuna wachezaji 42 wa klabu za ligi ya Uingereza miongoni mwa 100 bora akiwemo Eden Hazard wa Chelsea mwenye thamani ya pauni milioni 89, Anthony Martial wa Manchester United mwenye thamani ya pauni milioni 81, Raheem Sterling wa Manchester City mwenye thamani ya pauni milioni 75 na Jamie Vardy wa Leicester City mwenye thamani ya pauni milioni 45.
Kiungo wa kati wa West Ham Michail Antonio anafunga orodha ya wachezaji 100 wenye thamani ya juu akiwa na thamani ya pauni milioni 31.
No comments:
Post a Comment