Mchezaji bora zaidi Afrika mwaka 2016 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) atatangazwa leo jioni.
Wanaoshindania tuzo hiyo ni kiungo wa kati wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, winga wa Algeria Riyad Mahrez na winga wa Senegal Sadio Mané.
Mohamed Salah wa Misri na Islam Slimani wa Algeria walikuwa kwenye orodha ya wachezaji watano bora lakini wakashindwa kufika kwenye orodha ya wachezaji watatu bora.
Kwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika, kwa wachezaji wa ligi za mataifa ya Afrika, kipa wa Uganda Goal Keeper anashindana na mshambuliaji wa ZImbabwe Khama Billiat na iungo wa kati wa Zambia Rainford Kalaba .
Mshindi atatangazwa mjini Abuja, Nigeria saa 22.30 saa za Afrika Mashariki.
Wanaoshindania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika
- Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
- Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
- Sadio Mané (Senegal & Liverpool)
Wanaoshindania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika (Ligi za Afrika)
- Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
- Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)
- Rainford Kalaba (Zambia & TP Mazembe)
Washindi wa awali wa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika
2015: Pierre-Emerick Aubameyang
2014: Yaya Toure
2013: Yaya Toure
2012: Yaya Toure
2011: Yaya Toure
2010: Samuel Eto'o
2009: Didier Drogba
2008: Emmanuel Adebayor
2007: Frederic Kanoute
2006: Didier Drogba
2005: Samuel Eto'o
2004: Samuel Eto'o
2003: Samuel Eto'o
2002: El Hadji Diouf
2001: El Hadji Diouf
2000: Patrick Mbomba
1999: Nwankwo Kanu
1998: Mustapha Hadji
1997: Victor Ikpeba
1996: Nwankwo Kanu
1995: George Weah
1994: Emmanuel Amunike
1993: Rashidi Yekini
1992: Abedi Pele
No comments:
Post a Comment