Pages

Monday, January 2, 2017

Jose Mourinho achukizwa na Ivory Coast

Beki wa Manchester United Eric Bailey akizungumza na kocha Jose Mourinho

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionBeki wa Manchester United Eric Bailey akizungumza na kocha Jose Mourinho
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amechukizwa na Ivory Coast baada ya kumchukua beki Eric Bailey
Bailey alishiriki katika kikosi cha kwanza cha United katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesbrough na Mourinho alidhani beki huyo atajuimuika na wenzake katika mechi dhidi ya West Ham siku ya Jumatatu.
Mourinho ameambia mtandao wa klabu hiyo kwamba kocha Michel Dussuyuer alikuwa hayuko tayari kuchukua hatari yoyote wakati wanapojiandaa kutetea taji lao la Afrika.
''Baily anaondoka anaenda kuchezea timu yake ya taifa, alisema Mourinho. Ni lazima awe na timu yake mnamo tarehe 2 Januari. Tuliwaomba wamchukue tarehe 3 lakini wakakataa, kwa hivyo hawezi kucheza dhidi ya West Ham''.

No comments:

Post a Comment