TANGAZO


Monday, January 23, 2017

Claudio Ranieri: Meneja wa Leicester anataka Antonio Conte ashinde EPL

Claudio RanieriHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRanieri ndiye Mwitaliano wa tatu kushinda EPL baada ya Carlo Ancelotti (Chelsea mwaka 2009-10) na Roberto Mancini (Manchester City mwaka 2011-12)
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri amesema anataka sana Mwitaliano mwenzake Antonio Conte ashinde Ligi ya Premia na viongozi wa ligi wa sasa Chelsea.
Ranieri, 65, aliongoza Leicester kushinda ligi msimu uliopita kwa njia ya kushangaza.
Lakini kwa sasa Leicester wamo nambari 15 ligini, alama 34 nyuma ya klabu hiyo yake ya zamani.
"Kama mkufunzi wa zamani wa Chelsea na shabiki wa Italia, natumai Conte atatimiza lengo hilo," Ranieri amesema.
"Ameonesha kwamba makocha wa Italia ni stadi sana."
Ranieri ana mkataba Leicester hadi 2020 lakini anakubali kwamba nafasi yake katika klabu hiyo haiko salama, licha ya kufikia ufanisi wa kushangaza msimu uliopita.
"Natumai nitasalia England," aliongeza.
"Ninahisi vyema hapa, ingawa katika kandanda mnakuwa juu kwenye nyota leo na kesho yake mnajipata chini sakafuni, kwa hivyo usiwahi kudhania umefika."

No comments:

Post a Comment