Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee Na Watoto Dokta Mpoki
SERIKALI kupitia Wizarya afya , maendele ya jamii
, Jinsia Wazee na Watoto imetenga bilioni 251 ili kuimarisha upatikanaji wa
dawa katika vituo vya afya na zahanati zote nchini.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto
Dokta Mpoki wakati wa mahojiano katika kipindi cha Tunatekeleza kinachoendeshwa
na kituo cha matangazo TBC1 jijini Dar es salaam.
“Kutokana na taarifa zinazozagaa juu ya upungufu
wa dawa katika zahanati hapa nchini, taarifa hizo si za kweli napenda kuwatoa
hofu wananchi na bajeti yetu ya mwaka huu ni shilingi Bil. 251 kwa ajili ya dawa tu” alisema Dkt.
Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya alisisitiza kuwa kuna dawa
zitapewa kipaumbele kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa nchini ukilinganisha
na mahitaji ya dawa nyingine hivyo dawa zote zitaendelea kuwepo ili kuwasaidia
wananchi wote wenye uhitaji.
Dkt. Ulisubisya aliweka wazi juu ya mipango ya
serikali katika kuimarisha huduma za afya katika maeneo mbali mbali nchini ili
kujenga taifa lenye watu imara kiafya.
Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya amesema kuwa vituo vya serikali na vya watu binafsi ni
vyema viendelea kufuata sera, taratibu na sheria ikiwemo bei elekezi katika kuwahudumia
wananchi huduma bora kwa gharama ndogo.
Dkt. Ulisubisya amesisitiza kuwa Kufikia mwezi wa
tano mwaka huu asilimia 90 ya dawa zote zitakua zimepatikana na kusambazwa
kwenye vituo vya afya na zahanati zote nchini ili kuimarisha sekta ya afya na mpaka
sasa chanjo zote zipo za kutosha.
“Tunataka kila kituo cha afya kinachojengwa sasa
hivi kitoe huduma za upasuaji ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa wanahoitaji huduma hiyo na kuokoa
maisha ya mtanzania kwa haraka zaidi alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt Ulisubisya alisema kuwa Serikali ina
mkakati wa kuimarisha huduma zote za
vipimo ili zipatikane katika hospitali za wilaya na kikanda mpaka kufikia 2020
ili kuwezesha taifa kupiga hatua katika sekta ya afya.

No comments:
Post a Comment