TANGAZO


Monday, January 23, 2017

Arsenal yaishinda Burnley mabao 2-1


Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la piliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la pili

Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la pili dakika ya 98 kwa njia ya Penalti na kuiweza kuwashinda Burnley mabao 2-1 nyumbani mwa Arsenal huko Emirates.
Baada ya meneja wa Arsenal Arsene Wenger kutimuliwa uwanjani kwa kulalamikia uamuzi wa refa, kosa la Ben Mee la kumpiga kiatu Laurent Koscielny, lilisabaisha Burnley kuadhibiwa na Arsenal kupewa Penalti.
Arsenal walikuwa wameitawala mechi hadi pale Granit Xhaka alipotimuliwa baada ya kumchezea visivyo Steven Defour, hali iliyosababisha Burnley kunufaika.
Ushindi wa mara tano wa Arsenal katika uga wao wa Emirates, unawapandisha jedwali juu na Liverpool na Tottenham, ambao wote walipoteza pointi siku ya Jumamosi na kupunguza mwaya kati yao na Chelsea hadi pointi tano.

No comments:

Post a Comment