Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa
familia, ndugu, jamaa, wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia
kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku kilichotokea jana tarehe 23
Desemba, 2016 katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Nape Nnauye pamoja na
watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari
huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.
Mhe. Waziri Nape amepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo na ameeleza kuwa, kifo
chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha kwasababu Marehemu
wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times, The Guardian, Nipashe na Mwananchi
na The Citizen.
Wakati huo huo Mhe. Waziri ametuma
salamu za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na familia kufuatia kifo cha mtumishi
wake Bw. Modest Mfutakamba Mfilinge kilichotokea usiku wa kuamkia leo 24 Desemba,
2016.
Mungu azilaze roho za Marehemu mahali
pema peponi. Amina.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Dar es Salaam.
24 Desemba,
2016.


No comments:
Post a Comment