Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita.
Mdogo wa Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. (Picha zote na IKULU)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.
Rais Magufuli
pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao
pia amitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na
kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na
mifarakano.
''Unapotokea msiba
kama huu katika familia nyingi huzuka mifarakano, ombi langu kwenu wewe Mama
mkubwa na Mama mdogo kamwe msikubali kufarakanishwa kutokana na kifo cha mume
wenu,muwaongoze watoto wenu ili muendelee kuishi kwa kupendana kama enzi za
uhai wa mzee''
Aidha Rais
Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama kuwa alikuwa mzee maarufu kijijini
hapa na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare
zake za shule wakati akisoma.
Kwa upande wake
Mdogo wa marehemu ambaye ni msemaji wa familia Bwana Deodatus Manyama ambaye ni
msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli pamoja na ujumbe wake alioambatana
nao kuwapa pole katika msiba huo, na kwamba kitendo hicho kinaonyesha kuwa Rais
magufuli si mtu asiejikweza wala asiye na majivuno.
Marehemu Mzee
Admirabilis Mbabe Manyama amefariki akiwa na umri wa miaka 80,ameacha wajane
wawili,watoto 15 na wajukuuu kadhaa.
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato,
Geita.
29 Desemba,
2016
No comments:
Post a Comment