Sheria mpya inayowaruhusu maafisa wa polisi kuvaa vilemba badala ya kofia rasmi za polisi imezinduliwa mjini New York, maafisa wanasema.
Idara ya polisi mjini New York imesema kuwa vilemba hivyo ni shart viwe vya rangi ya buluu mbali na kumiliki chapa cha cha polisi wa New York NYPD.
Chini ya sheria mpya, wanachama wa dini ya kalasinga katika kikosi cha polisi pia wataruhusiwa kuweka ndevu zenye urefu wa nchi moja.
Maafisa Makalasinga wamekuwa wakivaa vilemba chini ya kofia zao rasmi. Ndevu hazikuwa zimeruhusiwa.
Kamishna wa mji wa New York James O'neil amesema kuwa mabadiliko hayo ni ya kuwavutia Makalasinga zaidi kutuma maombi ya kufanya kazi katika kikosi cha polisi mjini humo.
Muungano wa maafisa Makalasinga nchini Marekani umemshukuru O'neill katika chapisho la mtandao wa Twitter, ukiongezea kuwa ni fahari kubwa kwa jamii ya Makalasinga.
No comments:
Post a Comment