Pages

Tuesday, December 27, 2016

Polisi 29 washtakiwa kwa kutaka kuipindua serikali Uturuki

Askari waliohusika katika jaribio la mapinduzi nchini Uturuki washtakiwa
Image captionAskari waliohusika katika jaribio la mapinduzi nchini Uturuki washtakiwa
Takriban maafisa wa polisi 29 wanashtakiwa mjini Instabul Uturuki kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi mnamo mwezi Julai.
Kesi hiyo ndio muhimu zaidi kuwahi kufanyika huku zaidi ya mashtaka 1000 yakiandaliwa. Huku maafisa wengine 40 wakizuiliwa kesi hiyo inatarajiwa kuwa kubwa zaidi katika historia ya Uturuki ya leo.
Rais wa Uturuki katikati Reccep Tayip Erdogan
Image captionRais wa Uturuki katikati Reccep Tayip Erdogan
Washukiwa wanashtakiwa kwa kuwa na lengo la kuipindua serikali mbali na kujihusisha na kundi linaloongozwa na muhubiri anayeishi Marekani Fethullah Gulen, ambaye mamlaka inamlaumu kwa kupanga njama hiyo.

No comments:

Post a Comment