TANGAZO


Friday, December 30, 2016

Marekani yawafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi

Obama
Image captionRais wa Marekani, Barrack Obama
Rais Obama ameamuru kutimuliwa kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.
Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.
RUSSIAImage copyrightREUTERS
Image captionWadukuzi
Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa upande wake, rais mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia taarifa hizo za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushushu wa Marekani ili kulijadili hilo.
Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa kiwango hicho hicho.

No comments:

Post a Comment