Pages

Friday, December 2, 2016

Kina dada wa Cameroon kukutana na Nigeria nchini Yaoundé

Kikosi cha Cameroon
Fainali ya awamu ya kumi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada,imerudia matokea yake ya awamu ya tisa iliyochezwa nchini Namibia, ambapo Nigeria iliichapa Cameroon mabao 2-0.
Mechi ya fainali inatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Ahamadou Ahidjo, mjini Yaounde huku rais Paul Biya akitarajiwa kuwa miongoni mwa mashabiki wengi watakao hudhuria mechi hiyo.
Kina dada kutoka Nigeria Super Falcons wanatarajia kulitetea taji lao pia kupata ushindi kwa mara ya nane kati ya michuano 10 walioshiriki.
Timu ya Cameroon ya Indomitable Lionesses wanatafuta kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika Kombe la Taifa, mechi ambayo itakuwa mechi yao ya fainali ya tatu.
Timu hizo mbili zilipitia mashindano makali katika nusu fainali walitoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Cameroon wanatarajia kupata goli mmoja katika shindano hilo, huku Nigeria wamefunga magoli 12.
Florence OmagbemiImage copyrightGETTY IMAGES
Super Falcons wameziba nyavu yao na kukubali bao moja ambalo lilikuwa kupitia mkwaju wa penalti dhidi ya Ghana .
Cameroon wameingiza mpira nyavuni mara sita, lakini ilitarajiwa kuwa zaidi kutokana na umiliki wa mchezo waliouonyesha uwanjani.
Nahodha msimamizi wa Cameroon,Augustine Ejangue, amesema wachezaji chipukizi wa timu hiyo wako tayari kuminyana kwenye fainali na kunamshikamano halisi kwa kikosi chote hicho cha Cameroon.
Kocha wa Nigeria,Florence Omagbemi, anatarajia kuwa kocha mwanamke wa pili kushinda taji hilo. Omagbemi alishinda taji la kwanza kama nahodha. Amesema kikosi chake kiko tayari kiakili, kimwili na kisaikolojia kuhifadhi taji lao.
Asisat OshoalaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionAsisat Oshoala
Nyota wawili katika mashindano hayo ya soka ya kina dada nchini Afrika watakutana ana kwa ana kwenye fainali na mchezaji wa Nigeria na Arsenal Asisat Oshoala, akiongoza kikosi cha mashambulizi cha Super Falcons na Rosengard's Gaelle Enganamouit wa Cameroon ndio kiungo muhimu kwa Indomitable Lionesses na umati mkubwa wa mashabiki wataungana wakiwashabikia wenyeji Cameroon siku ya Jumamosi Mchana.

No comments:

Post a Comment