Jana Disemba 24, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa Bwana Godfrey Sinyangwe (kushoto) pamoja na Bi.Esther Kiluma (kulia), baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa la Saint Nicholas Jimbo Kuu la Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Lazaro Manjelenga aliyesaidiana na Mchungaji Joseph Samwel.
Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionesha matukio katika hafla ya ndoa hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo, ukumbi uliopo Bugando Jijini Mwanza.#BMG.
Maharusi wakikata keki.
Maharusi wakilishana keki, kwa upendo kabisa.
Best man wa bwana harusi, Kabuji Noah (kushoto) pamoja na Best lady wa bi.harusi, Huruma Ntangu (kulia) wakilishana keki.
Mshereheshaji, Mc.Lama, akifungua shampaini kwa ustadi wa hali ya juu.
Ndugu, jamaa, marafiki na wageni waaikwa wakiwapongeza maharusi.
Wazazi wa pande zote mbili wakiwa neno la wosia kwa maharusi.
Ndugu, jamaa, marafiki na wageni waalikwa wakitoa zawadi kwa maharusi.
Kapu la bibi kama kawaida.
Msosi ulipikwa kwa ustadi mkubwa.
Maharusi wakilishana chakula.
Wazazi wakipata chakula.
Ni wasaa wa kufungua mziki.
Burudani ikiendelea.
Hafla hii imefana sana, shukrani kwa wote waliofanikisha akiwemo Mwenyekiti wa sherehe, Erica Elias. BMG inawatakiwa kila la kheri kwenye ndoa yenu, Bwana Godfrey Sinyangwe pamoja na Bi.Esther Kiluma.
Tazama picha za ndoa HAPA















No comments:
Post a Comment