Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Bodi mpya
ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) aliyoizindua leo jijini Dar es Salaam. Wa
pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. John Kondoro.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akimkabidhi vitendea kazi
Mwenyekiti mpya wa bodi ya TRL, Profesa John Kondoro alipozindua bodi hiyo
jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa akimwonyesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, moja ya mabehewa
yaliyokarabatiwa na Kampuni hiyo alipotembelea karakana ya reli jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa akifafanua jambo wakati wa
Mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na
wafayakazi wa TRL alipoongea nao jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli
Tanzania (TRL), Masanja Kadogosa.Kulia ni Mwenyekiti ya Bodi ya TRL, Prof. John
Kondoro.
Wafanyakazi wa Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), alipoongea nao jana mchana jijiini Dar es Salaam.(Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)






No comments:
Post a Comment