Katibu Msaidizi toka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi akisisistiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari. Kulia ni Katibu msaidizi wa Tume hiyo, Bw. Peleleja Masele, kushoto ni Afisa Habari na Mawasiliano wa Tume hiyo, Bi. Jorlin Kagaruki.
Baadhi ya
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
Na Frank Mvungi-Maelezo
SERIKALI imewataka
watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ili kuleta ustawi kwa
wananchi kwa kutekeleza mipango
inayolenga kukuza uchumi na kutoa huduma bora.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya
Utumishi wa Umma Bw. Peleleja Masesa wakati wa mkutano na vyombo vya Habari.
Bw. Masesa amesema
kuwa Matokeo ya Makosa ya watumishi wa Umma waliokata rufaa Tume ya Utumishi wa
Umma mwaka 2014/2015 yanaonyesha kuwa kati ya watumishi 135 walikata rufaa
walipatikana na makosambalimbali ambapo 54 walipatikana na kosa la utoro
kazini.
Bw. Masesa aliongeza
kuwa watumishi wengine 16 walishindwa kutekeleza majukumu yao,10 kumdharau
mwajiri, 8 kughushi nyaraka mbalimbali,8 kufanya malipo kinyume na
taratibu, aidha makosa mengine yalikuwa chini ya watumishi 7.
Aidha Masesa aliwataka
watumishi wa Umma kujiepusha na vitendo vya rushwa, ulevi, utoro makazini na
matendo yote yanayokwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
“Utendaji kazi
katika utumishi wa Umma huongozwa na sheria, kanuni, taratibu na Miongozo
mbalimbali ambayo ipo.” Alisisitiza Masesa.
Pia Masesa amesema kuwa watumishi watakaoshindwa
kuzingatia taratibu zilizowekwa watachukuliwa hatua kali za kisheria na mamlaka
za nidhamu katika taasisi husika.
Tume ya Utumishi wa
Umma, inawataka waajiri, Mamlaka za ajira na nidhamu na Watumishi wote kuzingatia
kanuni za maadili wakati wote wanapotekeleza majukumu yao ili kukuza
uchumi, kutoa huduma bora kwa jamii na kulinda amani na utulivu wa nchi.
No comments:
Post a Comment